MKUU WA WILAYA YA KIBAHA AWATAKA WATOA HUDUMA WATEKELEZE WAJIBU WAO KWA WELEDI.
Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mhe. Martin Mtemo amewataka watumishi waliopangwa kwenye Hospitali mpya ya Wilaya kuwahudumia wananchi kwa weledi na kutokuruhusu malalamiko ya aina yoyote kutoka kwa wagonjwa na kuepuka vitendo vya rushwa .
Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo alipokuwa akizindua hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Kibaha iliyojengwa Disunyara Mlandizi kwa gharama ya 1.7bilioni ikiwa na majengo 7.
Pamoja na hayo Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya kibaha Butamo Ndalahwa amesema wanaendelea kushirikiana na DAWASA ili kuhakikisha hospital hiyo inapata maji pamoja na changamoto ya kuwa line ya maji waliyounganishwa nayo ina watumiaji wengi sana hivyo wanashirikiana na dawasa ili waweze kubadilishiwa line nyingine ili kuhakikisha hospital inapata maji masaa 24
Butamo amemuomba Mkuu wa Wilaya kuwasaidia kuongea na Sumatra ili ipatikaneroute ya daladala ya kwenda hospitali ya Wilaya ili kupunguza gharama za usafiri kwa wagonjwa watakaoenda kupata huduma kwenye hospitali hiyo .
Mganga mfawadhi wa hospitali hiyo amesema pamoja na hospitali hiyo kufunguliwa bado kuna changamoto ya dawa na vifaa tiba pamoja na makazi ya watumishi.
Wananchi waliofika kupata huduma kwenye Hospitali hiyo wameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuwaletea hospitali ya wilaya kwani walikuwa wanahangaika sana kufuata huduma Tumbi pale mgonjwa anapopewa rufaa kutoka kituo cha afya Mlandizi.
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.