MWAKAMO ARIDHISHWA NA MATUMIZI YA FEDHA
Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani Michael Mwakamo ,amefanya ziara ya kukagua matumizi ya Tsh Milioni 68 zilizochangishwa na Rais Dkt John Magufuli katika Kijiji cha Soga.
Ikiwa ni ziara yake ya kwanza jimboni hapo, alijionea matumizi mazuri ya fedha alizochangisha Rais Magufuli alipopita kijijini hapo miezi michache iliyopita akitokea kwenye ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa wa reli ya kisasa ya SGR inayopita Soga.
Akiwa Shuleni hapo alipokelewa na mwalimu mkuu msaidizi Catherine Mganga na Mwenyekiti wa Kijiji Fadhili Lihamba aliyemwelezea Rais uwepo wa changamoto katika shule hiyo,ambapo alikagua majengo hayo kabla ya kuzungumza na viongozi na walimu hao.
Alisema hana budi kufuatilia maagizo anayoyatoa ikiwemo fedha anazozichangisha au kuzipeleka katika miradi mbalimbali ,ili kujiridhisha na matumizi yake ndiyo maana ziara yake ya kwanza akaanzia Soga.
“Mbunge wenu nimeamua kufanya ziara yangu ya kwanza toka niapishwe kushika wadhifa huu kuja kukagua matumizi yay a fedha zilizochangishwa na Rais Magufuli , niseme nimeridhishwa na matumizi yake ,majengo yamekidhi viwango hongereni sana “alisema Mwakamo.
Aliwataka mafundi kuhakikisha kwamba ukarabati huo wa vyumba uende sambamba na ukarabati wa sakafu..
Kwa Upande wa Lihamba alimshukuru ,Rais Magufuli kwa kuguswa na changamoto ya uchakavu wa vyumba hivyo kwamba shule hiyo sasa inapendeza .
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.