Majukumu ya Idara ya Afya Kusimamia shughuli zote za utoaji wa huduma za Afya kwa kufuata miongozo na seraza afya na ubora unaohitajika ,pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu masualayote yahusuyo afya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali. Kuandaa Mpango kabambe wa Afya wa mwaka na kutoa taarifa za utekelezaji washughuli za afya kama zilivyo ainishwa katika Mpango na kuziwasilisha katika mamlakahusika. Kufanya ziara za usimamizi na ufuatiliaji wa utaoji wa huduma za afya katika vituo vyotevya kutolea huduma za afya katika Wilaya. Kusimamia usambazaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vyote vyahuduma Wilayani na kuhakikisha dawa zinakuwepo vituoni. Kubuni na kutayarisha mikakati ya kuinua ubora wa huduma ya Afya. Kutoa huduma za outreach na mobile kliniki katika kuboresha utoaji wa huduma za Afya. Kusimamia watumishi wa Afya na kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa kuzingatiamaadili ya kazi, kanuni na miongozo mbalimbali zinazosimamia utendaji wa watumishi, Kusimamia rasilimali na nyenzo za kuendesha huduma zote za Afya na kuzitunza. Kuhamasisha jamii kuchangia huduma za Afya na kushiriki katika kampeni mbalimbaliza Afya.
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.