1.0: JIOGRAFIA YA WILAYA
1.1: Mipaka Na Eneo
Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha iko umbali wa kilometa 40 toka Jiji la Dar es salaam kando kando ya barabara kuu iendayo Morogoro. Halmashauri ya Wilaya inapatikana kati ya latitudi 6-8 Kusini mwa Ikweta na Longitudi 38.0 hadi 39.05 Mashariki. Kaskazini inapakana na Wilaya ya Bagamoyo, na Kusini inapakana na Wilaya ya Kisarawe, upande wa Mashariki inapakana na Halmashauri ya Mji wa kibaha, Upande wa Magharibi inapakana na Wilaya ya Bagamoyo na Wilaya ya Morogoro.
1.2: Utawala / Eneo
Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha ina jumla ya Tarafa 2 na Kata 14. Tarafa ni Mlandizi na Ruvu,Kata zake ni Kwala, Ruvu, Magindu, Mlandizi, Soga, Janga, Kilangalanga, Gwata, Bokomnemela, Dutumi, Kikongo, Kawawa, Mtongani, na Mtambani. Ikiwa na jumla ya Vijiji 25 na Vitongoji 100. Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha ina eneo la ukubwa wa Hekta 124,217.755 sawa na kilometa za mraba 1992.18
1.3: Mipaka
Halmashauri ya Wilaya inapatikana kati ya latitudi 6-8 Kusini mwa Ikweta na Longtudi 38.0 hadi 39.05 Mashariki. Kaskazini inapakana na Wilaya ya Bagamoyo, na Kusini inapakana na Wilaya ya Kisarawe, upande wa Mashariki inapakana na Halmashauri ya Mji wa kibaha, Upande wa Magharibi inapakana na Wilaya ya Bagamoyo na Wilaya ya Morogoro.
1.4: Idadi Ya Watu
Kwa mujibu wa Sensa ya watuna makazi mwaka 2012, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha ina jumla ya Kaya 17,124 na watu wapatao 70,209 ikiwa ni ongezeko la asilimia 2.2 Jedwali lifuatalo linaonyesha mchanganuo wa idadi ya watu katika kila Kata kijinsi, wastani kwa kaya na uwiano kijinsia.
JEDWALI NA. 1: IDADI YA WATU KWA KATA
KATA |
JUMLA YA WATU |
ME |
KE |
WASTANI KWA KAYA |
UWIANO KIJINSIA |
Gwata
|
5,280 |
2,585 |
2,695 |
4.7 |
96 |
Dutumi
|
1,812 |
939 |
873 |
4.2 |
108 |
Magindu
|
4,991 |
2,453 |
2,538 |
4.5 |
97 |
Soga
|
4,713 |
2,428 |
2,285 |
3.7 |
106 |
Kikongo
|
4,238 |
2,112 |
2,126 |
3.7 |
99 |
Ruvu
|
3,466 |
1,719 |
1,747 |
3.8 |
98 |
Mlandizi
|
17,318 |
8,546 |
8,772 |
4.2 |
97 |
Kwala
|
3,472 |
1,749 |
1,723 |
3.8 |
102 |
Kilangalanga
|
10,588 |
4,997 |
5,591 |
4.3 |
89 |
Janga
|
10,926 |
5,242 |
5,684 |
4.0 |
92 |
Bokomnemela
|
3,405 |
1,745 |
1,660 |
3.8 |
105 |
Total
|
70,209 |
34,515 |
35,694 |
4.1 |
97 |
Chanzo: Sensa ya Watu na Makazi Tanzania, 2012.
1.5: Hali ya Hewa
Wilaya ina misimu miwili ya mvua, Vuli miezi ya Novemba na Desemba na Masika miezi ya Machi hadi Aprili. Wastani wa mvua kwa mwaka ni mm 800. Wastani wa joto ni nyuzi joto 29.7 na wastani wa unyevu unafikia 56%.
3.0: HALI YA MAENDELEO YA HALMASHAURI YA WILAYA
3.1: Hali ya kiuchumi na kijamii
Halmashauri ya Wilaya Kibaha ina wakazi wachache waliosambaa katika maeneo mbalimbali isipokuwa Mji wa Mlandizi wenye wakazi wengi. Mji wa Mlandizi unakua haraka ukiwa na watu wa Tabaka mbalimbali na tamaduni zinazotofautiana. Ukaribu wake kutoka Mji Mkuu wa kibiashara Dar es Salaam unachangia kwa kiasi kikubwa. Mabadiliko ya kijamii na kiutamaduni hasa kutoka nchi za Kimagharibi.
Mlandizi inazo Taasisi nyingi za Umma na Binafsi zinazosaidia kutoa ajira kwa wakazi. Hizi ni pamoja na shule za Msingi na Sekondari, JKT na Idadi kubwa ya wafanyabiashara kama maduka ya jumla, rejareja, migahawa, mama lishe vilabu vya pombe za kienyeji, viwanda vidogo kama upasuaji wa mbao, ushonaji, usagishaji n.k.
Shughuli za kiuchumi katika Halmashauri ya wilaya Kibaha ni kilimo, ufugaji ukiendeshwa zaidi na makabila ya Kimasai na Mang’ati hususani katika Kata za Kwala na Magindu. Ipo idadi ndogo ya wakazi wanaoendesha ufugaji wa kisasa wa kuku na ng’ombe wa maziwa. Mazao makuu ya kilimo ni Korosho, Ufuta, Machungwa, kilimo cha mbogamboga kama Matango, Nyanya, Pilipilli, Bilinganya, Matikiti maji n.k, kwa asilimia kubwa kilimo hiki hufanyika katika Bonde la Mto Ruvu. Mazao ya chakula ni pamoja na Mhogo, Mpunga, Mtama na Mahindi.
Shughuli za kilimo kwa kiasi kikubwa ni kwaajili ya kujikimu kwa chakula, ni watu wachache tu, hususani Mlandizi wako waajiriwa katika Taasisi za Umma na Binafsi kwa shughuli hii. Baadhi ya wakazi wanajishughulisha na uvunaji wa mazao ya Misitu kwa ajili ya ujenzi, kuni na uchomaji mkaa, kwa kiwango kidogo pia hujishughulisha na ufugaji na uvunaji wa mazao ya nyuki.
Huduma za jamii zinazopatikana ni Afya, Elimu, Maji na Barabara. Mafanikio yote haya ni juhudi zinazofanywa na Halmashauri ya Wilaya Kibaha.
15.0: MWISHO
Kwa mujibu wa taarifa hii, Wilaya imekuwa na mafanikio ya kuridhisha katika kuboresha hali ya maisha ya wananchi wake kupitia utoaji wa huduma za Kijamii za Elimu, Afya, Maji na huduma za kiuchumi za Barabara, Madaraja, Majengo; Kilimo, Uvuvi, Mifugo, Utalii, Biashara, Mawasiliano na Ardhi. Aidha, huduma ya Utawala bora imeongezeka pamoja na kudumisha hali ya amani, ulinzi na usalama wa raia na mali zao. Mafanikio haya yametokana na ushirikiano mzuri baina ya uongozi wa Chama na Serikali Wilayani, watendaji wa Wilaya, Taasisi, Wananchi na Wadau mbalimbali Wa Maendeleo hapa wilayani Kibaha.
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.