Majukumu ya Idara ya maji
Kutafsiri na kusimamia sera za Wizara ya Maji katika ngazi ya Halmashauri ya Wilaya.
Kusimamia, kufanya utafiti na kutoa mapendekezo ya namna ya kukabiliana na matatizo mbalimbali yanayorudisha nyuma huduma ya upatikanaji wa maji.
Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Halmashauri ya Wilaya, mashirika yasiyo ya kiserikali, binafsi na kidini kuhusu namna ya kushirikiana kukabili tatizo la upatikanji wa huduma ya maji ndani ya Wilaya.
Kusimamia na kuratibu miradi yote ya maji ndani ya wilaya,
Kuandaa Bajeti ya mwaka ya Mishahara, shughuli za uendeshaji na Miradi ya Maendeleo kwa upande wa Idara ya maji,
Kutoa ushauri kwa serikali kuhusu Sera ya Sekta ya Maji na kudurusu sera, sheria na kanuni zake, na
Kuratibu na kushauri mfumo wa matumizi bora ya miradi ya maji ili iwe endelevu.
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.