Majukumu ya Kitengo cha Usafishaji Na Mazingira
Idara ya Usafishaji inatekeleza majukumu yafuatayo;
Utekelezaji Usafishaji Na Mazingira
Idara ya Usafishaji ina shughuli za usafi wa majengo; usafi wa maeneo ya wazi; barabara; na mifereji, usafishaji uchambuaji na utupaji taka kisasa (Sanitary Land fill-Dampo).
6.3.1: Uzoaji wa taka ngumu
Katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mlandizi taka ngumu hukusanywa na Kikosi Kazi (GEOBEST) kwa kushirikiana na vibarua wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha katika maeneo ya Kata ya Mlandinzi; Kilangalanga, Mtambani na Janga kwa kufagia, kukusanya, kuzoa na kutupa dampo la muda lililopo eneo la Disunyara. Kata zingine zilizo pembezoni mwa mji mdogo wa Mlandizi jamii hufagia na kukusanya taka yenyewe na kutupa kwenye mashimo ya takataka kwani miundombinu ya kata hii hali inaruhusu kufanya hivyo. Halmashauri inalo trekta kwa ajili ya uzoaji taka lenye ukubwa wa tani 4 na wakati mwingine trekta linaposhindwa kuifikia mitaa yote kwa ajili ya uzoaji halmashauri kukodi magari mara mbili (2) kila wiki kwa ajili ya kuondoa taka ngumu ambazo hazikufikiwa na trekta. Mlandizi inazalisha takribani tani 24 za taka ngumu kila siku. Na Trekta lina uwezo wa kusomba tani 12 tu za taka ngumu kwa siku.
Pia shughuli za usafi na ukaguzi wa majengo hufanywa na maafisa katika kata zao na maeneo mengine waliopangiwa. Kampeni ya Usafi wa Mazingira huwa ikifanyika siku ya alhamisi ya kila mwisho wa mwezi, Halmashauri yetu imeiteua siku hiyo kuwa ni siku pekee ya kufanya Usafi wa Mazingira katika makazi, barabarani na taasisi mbalimbali na maeneo mengine ya wazi Kwa kushirikiana na Watendaji/wataalamu, viongozi na wananchi. Siku ya usafi wa mazingira katika halmashauri ya Kibaha ilizinduliwa rasmi tarehe 26/03/2015 ili kuifanya jamii iweze kubadili tabia mbaya ya uchafuzi wa mazingira na kuwa na tabia ya ustaarabu wa utunzaji wa mazingira na kutambua kwamba jukumu la usafi wa mazingira sio la idara husika ila ni la jamii nzima.
6.3.2: Upande Wa Utunzaji Mazingira
Idara imefanya shughuli za udhibiti wa uchafuzi wa ardhi, maji, hewa, na sauti. Utunzaji na upendezeshaji mazingira unaohusiana na kupanda miti na maua, kukatia miti na majani pia usimamizi wa ufuatiliaji wa tathimini ya athari za mazingira katika shughuli mbalimali za maendeleo.
6.3.3: Mafanikio Ya Usafi Wa Mazingira
.
6.3.4: Changamoto
6.3.5: Utatuzi Wa Changamoto
Kwa upande wa ufinyu wa bajeti halmashauri hutumia vyanzo vyake vya mapato ya ndani ili kukabiliana na changamoto hiyo. Idara hutumia watumishi wa idara ya afya na ustawi wa jamii pamoja na watumishi wa misitu ili kukabiliana na tatizo la upungufu mkubwa wa watumishi uliopo katika idara.
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.