Utekelezaji Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji;
Idara ya mipango na takwimu inajumuisha wataalamu wa mipango na takwimu ambao kwa ujumla wanasimamiwa na Afisa mipango wa wilaya. Idara ya mipango ndiyo inayoratibu shughuli zote za miradi ya maendeleo pamoja na kuandaa taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi hiyo mfano taarifa za robo mwaka, taarifa za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi, uratibu wa uandaaji wa bajeti na utekelezaji wake, n.k. Taarifa hizi hupelekwa ngazi za juu kwa ajili ya ufuatiliaji zaidi.
Majukumu ya idara hii kiutawala yameainishwa kuonesha majukumu ya mtakwimu na majukumu ya wachumi/mipango ila katika utekelezaji majukumu haya hutekelezwa kwa pamoja. Pamoja na kuahinishwa kwa majukumu hayo, pia Idara kwa mujibu wa waraka mpya wa muundo wa Idara za Halmashauri, Idara ina sehemu kuu tatu;
Majukumu ya Mipango (Sera na Mipango & Tathmini na Ukaguzi wa Miradi)
Kuratibu masuala yote ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Kuandaa mpango na taarifa za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha tawala kwa kipindi cha miaka mitano,mwaka mmoja na nusu mwaka.
Kufanya tathmini na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ili kubaini ubora wa mradi na thamani ya fedha iliyotolewa (value for money)
Kuratibu miradi iliyofadhiliwa na Wahisani wilayani.
Kuratibu Mipango na Bajeti ikiwemo Mpango Mkakati na Mipango kazi ya wilaya.
Kuunganisha, kuratibu na kufuatilia Mipango na Bajeti za Serikali za mitaa.
Kushiriki katika kufuatilia, kukagua na kutoa tathmini kwenye miradi ya maendeleo wilayani ili kupata takwimu sahihi za utekelezaji wa kazi za serikali.
Kushiriki katika kuandaa taarifa za utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kuratibu shughuli za tafiti zote wilayani, ikiwa ni pamoja na kufanya tafiti za kina kuhusu vyanzo vya mapato vya Halmashauri.
Kuchapisha machapisho mbalimbali ya kiucumi na kijamii wilayani.
Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa mkataba wa huduma kwa wateja.
Idara ya Mipango ndiyo Sekretarieti katika vikao vya Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC).
Kuratibu masuala ya Maafa katika wilaya.
Kazi Za Mtakwimu Wa Halmashauri
Mtakwimu wa Halmashauri anashiriki katika kazi zote za kitakwimu zinazofanyika katika halmashauri. Mtakwimu anafanya kazi chini ya usimamizi wa Afisa Mipango Wilaya. Kazi za mtakwimu wa wilaya ni kama ifuatavyo;
Kushirikiana na idara zote za kisekta (kwa mafano Afya, Elimu, Kilimo, n.k) ndani ya Halmashauri ili kuwa na mfumo mzuri wa kitakwimu.
Kuandaa mkusanyiko wa takwimu za kiuchumi na kijamii“(Socio economic profile),
Kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakati wa zoezi la Sensa ya idadi ya watu na Makazi.
Mtakwimu pia ni mwenyekiti wa kikundi kazi cha ukusanyaji wa takwimu ndani ya Halmashauri (District Statistics Working Group).
Kufuatilia mwenendo wa mfumo wa utunzaji wa takwimu katika ngazi ya serikali za mitaa(LGMD) na kushirikiana na idara nyingine zenye mifumo mingine ya utunzajia wa takwimu za kisekta kwa mfano;
Maliasili - NAFOBEDA, Afya - MTUHA na Elimu - BEST.
LGMD - Local Government Monitoring database, BEST-Basic Education Statistics na NAFOBEDA - National Forestry and Beekeeping Database.
JEDWALI NA. UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU IDARA YA MIPANGO
NA.
|
UTEKELEZAJI |
||
Utekelezaji kwa Vitengo vya Mipango & Sera; Mipango & Tathmini na Ukaguzi wa Miradi |
|||
|
Kuratibu masuala ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
|
Idara imekuwa ikishirikiana na Idara zingine kuboresha na kuinua maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa kuendelea kuboresha miradi ya maendeleo.
|
|
|
Kuandaa Mpango na Taarifa za Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa kipindi cha Miaka mitano, mwaka mmoja na nusu mwaka.
|
Taarifa ya Utekelezaji Ilani ya Chama kwa kipindi cha cha mwaka mmoja na ile ya Miaka mitano zote huandaliwa na kuwasilishwa Mkoani, ambapo Taarifa ya Miaka Mitano iliwasilishwa kwa barua yenye KUMBUKUMBU NA. KDC/A. 160/41/39 ya tarehe 06 August, 2015.
|
|
|
Kufanya tathmini na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ili kubaini ubora wa mradi na thamani ya fedha iliyotolewa (value for money).
|
Idara kwa kushirikiana na Idara za Maji, Kilimo, Mifugo na Ujenzi, hufanya ziara za ukaguzi katika miradi yote. Miradi iliyokaguliwa ipo kwenye ubora unaotakiwa.
|
|
|
Kuratibu miradi iliyofadhiliwa na Wahisani wilayani.
|
Idara hutekeleza uratibu wa miradi inayofadhiliwa na wahisani kwa kushirikiana na Idara husika.
|
|
|
Kuratibu Mipango na Bajeti ikiwemo Mpango Mkakati na Mipango kazi ya wilaya.
|
Bajeti, Mpangomkakati, pamoja na Mpangokazi wa Halmashauri huandaliwa kwa wakati na kuwasilishwa mamlaka za juu kwa mujumuisho ya kitaifa. Kwa sasa utekelezaji wake unaendelea. Aidha, mchakato wa Bajeti, Mpangomkakati, na Mpangokazi kwa mwaka mpya wa fedha wa 2016/17 upo katika hatua za mwisho.
|
|
|
Kuunganisha, kuratibu na kufuatilia Mipango na Bajeti za Serikali za mitaa.
|
Ufuatiliaji unafanyika na utekelezaji unaendelea
|
|
|
Kushiriki katika kufuatilia, kukagua na kutoa tathmini kwenye miradi ya maendeleo wilayani ili kupata takwimu sahihi za utekelezaji wa kazi za serikali.
|
Ufuatiliaji ni jukumu endelevu ambapo hufanyika kwa kila mwisho wa robo mwaka, miradi inakaguliwa na taarifa huwa zinawasilishwa ofisi ya mkurugenzi.
|
|
|
Kushiriki katika kuandaa taarifa za utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo.
|
Maandalizi ya taarifa kwa vipindi vya robo mwaka hufanyika na taarifa kuwasilishwa kwenye kikao cha Kamati za kudumu kwa mujibu wa sheria katika kikao cha tarehe 21 Oktoba, 2015.
|
|
|
Kuratibu shughuli za tafiti zote wilayani, ikiwa ni pamoja na kufanya tafiti za kina kuhusu vyanzo vya mapato vya Halmashauri.
|
Mpaka sasa tafiti zilizofanyika ni pamoja na tafiti ndogo za vyanzo vya mapato katika ushuru wa;
|
|
|
Kuchapisha machapisho mbalimbali ya kiucumi na kijamii wilayani.
|
Zoezi la uandaaji machapisho linaendelea. Kwa sasa Idara inajiandaa kuhuisha taarifa za machapisho ya ‘Council Socio-Economic Profile’ na ‘Council Investment Profile’.
|
|
|
Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa mkataba wa huduma kwa wateja.
|
Zoezi la kuhuisha Mkataba wa Huduma kwa Wateja hufanyika kwa kushirikiana na Idara ya Utumishi.
|
|
|
Idara ya Mipango ndiyo Sekretarieti katika vikao vya Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC).
|
Jukumu hili hufanyika kama utaratibu unavyoelekeza.
|
|
|
Kuratibu masuala ya Maafa katika wilaya.
|
Jukumu hili hufanyika kama utaratibu unavyoelekeza.
|
|
Utekelezaji kwa Kitengo cha Takwimu Wa Halmashauri |
|||
1.
|
Kusimamia kitengo cha Takwimu katika Halmashauri Kukusanya, kuchambua, kutafsiri na kuwasilisha takwimu ili ziweze kutumika katika mipango ya Halmashauri.
|
Zoezi la ukusanyaji takwimu linaendelea tatizo kubwa ni uhaba wa fedha. Idara inashauri kuwa, ruzuku kutoka serikali kuu na fedha za wahisani ziwe zinafika kwa wakati.
|
|
2.
|
Kushirikiana na idara zote za kisekta (kwa mafano Afya, Elimu, Kilimo, n.k) ndani ya Halmashauri ili kuwa na mfumo mzuri wa kitakwimu.
|
Zoezi la ukusanyaji takwimu linaendelea tatizo kubwa ni uhaba wa fedha. Idara inashauri kuwa, ruzuku kutoka serikali kuu na fedha za wahisani ziwe zinafika kwa wakati.
|
|
3.
|
Kuandaa mkusanyiko wa takwimu za kiuchumi na kijamii“(Socio economic profile).
|
Taarifa za awali zilizokusanywa ni pamoja na ‘Socio-Economic Profile’ na ‘Investment Profile’. Idara inaendelea na kuzihuisha takwimu hizi ili ziweze kuingizwa katika mfumo wa serikali kwa matumizi ya ngazi za juu. Zoezi linatekelezwa kwa kusua kusua kutokana na uhaba wa fedha. Idara inashauri kuwa, ruzuku kutoka serikali kuu na fedha za wahisani ziwe zinafika kwa wakati.
|
|
4.
|
Kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakati wa zoezi la Sensa ya idadi ya watu na Makazi.
|
Zoezi hili hufanyika kila baada ya miaka 10, mara ya mwisho lilifanyika 2012 hivyo litafanyika tena 2022.
|
|
5.
|
Mtakwimu pia ni mwenyekiti wa kikundi kazi cha ukusanyaji wa takwimu ndani ya Halmashauri (District Statistics Working Group).
|
Hatuna Kikundi kazi cha aina hii katika halmashauri ya Wilaya ya Kibaha.
|
|
6.
|
Kufuatilia mwenendo wa mfumo wa utunzaji wa takwimu katika ngazi ya serikali za mitaa (LGMD) na kushirikiana na idara nyingine zenye mifumo mingine ya utunzajia wa takwimu za kisekta
|
Zoezi halijafanyika kutokana na ukosefu wa fedha.
|
|
Utekelezaji wa majukumu mengine
|
|||
1
|
Maagizo kutoka serikali kuu
|
Idara imekuwa ikitekeleza maagizo yote kutoka serikali kuu moja kwa moja, maagizo yatokanayo na ziara za viongozi wa kitaifa na Maagizo yatokanayo na hotuba mbalimbali za viongozi. Taarifa zake huandaliwa na kuwasilishwa kwa Katibu Tawala (M).
|
|
2
|
Maagizo ya Mkurugenzi
|
Maagizo ya Mkurugenzi yanatokana na maazimio ya vikao mbalimbali vya kamati za kudumu za waheshimiwa madiwani, hivyo Idara imekuwa ikitekeleza kadiri inavyowasilishwa.
|
|
|
|
|
|
Changamoto
Changamoto kubwa inayoikabili Idara ni uhaba wa fedha, ambapo idara inaendelea na kuandika maandiko ya kutafuta fedha zitakazosaidia utekelezaji wa miradi. Maandiko hayo ni pamoja na uuzwaji wa hatifungani za halmashauri.
Malengo Ya Baadae
Pamoja na utekelezaji wa majukumu hayo, Idara ina malengo ya kutekeleza yafuatayo kadiri ya upatikaji wa fedha;
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.