Wajumbe tisa kutoka nchi ya Angola wamefanya ziara ya kujifunza na kubadilishana uzoefu katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha ambapo walitembelea miradi pamojana kukutana na wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya za walengwa unaotekelezwa na Mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF)Wajumbe hao kutoka nchini Angola wametembelea Tanzania kwa lengo la kujifunza,utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAFAkiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mpango ngazi ya Halmashauri Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauriya Wilaya ya Kibaha Butamo Ndalahwa ameeleza kuwa kuanzia kipindi cha malipo cha Juli- Agosti 2020 hadiNovemba - Disemba 2022, Tshs. Bilioni 1.4 kutoka TASAF zimepokelewa kwa ajili ya malipo ya wanufaika pamoja na ufuatiliaji nausimamizi.Ndalahwa amesema TASAF inawanufaika katika vijiji 46 vya Halmashauri hiyo nakwamba kutokana na fedha zinazotolewa kaya za wanufaika zimeweza kujikwamuakiuchumi kwa kuanzisha shughuli za kuongeza kipato ikiwa ni pamoja na kilimo, ufugaji na biashara ndogondogo.Awali kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Nsajigwa Mwamunyange ameelezeanamna walivyofurahishwa na wajumbe hao kufanya ziara yao hapa nchini hususaniMkoa wa Pwani.Nsajigwa ameeleza kuwa TASAF imesaidia utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleona kubadilisha maisha ya wanufaika kutoka kaya za walengwa kwani Serikali peke yakeisingeweza kufikia maeneo yote.Mkurugenzi msaidizi Rosa Teixeira Decarvalho kutoka FAS Carvalho amesemaamefurahishwa na utekelezaji wa miradi ya TASAF, pamoja na ushuhuda kutoka kwawanufaika ikiwemo eneo la elimu.Rosa amesema wajumbe hao tisa kutoka Serikali ya Angola pia wamefurahishwanamna jamii inavyoshiriki katika shughuli za miradi ya TASAF, lakini pia utekelezaji wamiradi ikiwemo ya barabara ambayo inarahisisha usafiri kwa wananchi.Wajumbe hao walitembelea miradi ya bwawa la maji na barabara iliyotekelezwa naTASAF, pamoja na kusikiliza shuhuda za wanufaika katika kijiji cha VikugeAmina Ally na Selemani Mgomba ni kati ya wanufaika kutoka katika Kijiji cha Vikugeambao wameishukuru TASAF kwa namna ilivyowawezesha kubadilisha maisha yao.Ashura Said amesema kupitia Mfuko wa TASAF
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.