Halmshauri ya wilaya ya Kibaha, Mkoani Pwani imejipanga kuimarisha makusanyo ya ushuru wa mauzo ya viwanja na kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha kwenye vyanzo mbalimbali.
Aidha ,imejipanga kuwachukulia hatua za kisheria wale watakaobainika kusababisha upotevu wa fedha na kukwepa kulipa ushuru.
Akielezea mkakati huo ,wakati wa Baraza la madiwani ,Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha ,Arasto Mpangala Makala ameeleza, kipindi cha nyuma hawakufanya vizuri Ila wanashukuru kwa ushirikiano,ufuatiliaji na usimamizi mzuri wa mapato umesaidia Halmashauri sasa imekuwa ya kwanza Kitaifa kwa kukusanya asilimia 247 ya makisio yake ya mwaka.
Makala amefafanua hadi kufikia June 30 mwaka huu walikusanya Bilioni 28.6 sawa na asilimia 68 ya lengo kati ya fedha hizo walikuwa na Bilioni 3.8 ambazo ni mapato ya ndani ya vyanzo vya masharti na visivyo vya masharti.
Nae Mbunge wa Viti Maalum Mkoani Pwani,Hawa Mchafu ameitaka Halmashauri hiyo kusimamia miradi ya maendeleo na kuhakikisha inamalizika kwa wakati .
Akichangia hoja, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ,Josephina Gunda alielezea kwamba ,chanzo Cha stendi ,mkaa,minada na mchanga haikufanya vizuri ,kwasasa wamejielekeza kufanya ufuatiliaji na kubadilisha mfumo wa ukataji ushuru kwa kuwabana wakata ushuru ambao sio waaminifu.
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.