Kamati ya siasa ya Halmashauri ya wilaya ya Kibaha imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Halmashauri.
Miradi iliyokaguliwa na kamati hiyo ni pamoja na mradi wa umwagiliaji wa mwangomole unaopatikana kata ya Kwala , mradi huu uliibuliwa na jamii ya kwala mwaka 2006 kupitia mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo Wilaya (DADPs). Lengo kuu ilikuwa ni kutengeneza miundombinu ya umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji wa zao la mpunga. Mradi huu mpaka sasa umegharimu Tsh 1,174,960 na wakulima wameanza kulima.
Mradi mwingine uliotembelewa ni mradi wa maji Kwala ambao unasimamiwa na Ruwasa Kibaha mradi huu unahusisha ujenzi wa tanki la maji lita 500,000 kwenye mnara wa mita 12, ujenzi wa nyumba ya mashine na vituo 12 vya kuchotea maji .mradi huu hadi kukamilika utagharimu Tsh 1,436,546 na unatarajiwa kuhudumia wananchi 9,500 kata ya kwala imekuwa na changamoto ya maji kwa kipindi kirefu hivyo mradi huu utakuwa mkombozi kwa wananchi wa kwala.
Mwenyekiti wa Ccm Kibaha ameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe. Samia Suluhu Hasan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwakumbuka watu wa Kwala kwani suala la maji katika kata hiyo ni kero kubwa.
Pia kamati ilitembelea ujenzi wa kituo cha afya kwala kinachojengwa kwa fedha za tozo jumla ya milioni 500 zimepokelewa kutoka serikali kuu kwa awamu mbili awamu ya kwanza Halmashauri ilipokea milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la OPD na maabara na awamu ya pili milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wazazi , upasuaji pamoja na jengo la kufulia.
Kamati ya siasa imewapongeza watendaji kwa usimamazi mzuri wa ujenzi wa majengo hayo kwani thamani ya fedha inaonekana.
Ujenzi wa madarasa manne shule ya msingi Madege kwa gharama ya milioni 112,500,000 ulitembelewa na kamati ya siasa . kamati hiyo iliendelea kupongeza juhudi za serikali katika kuboresha miundombinu ya elimu kwani shule ya Msingi Madege madarasa yao yalikuwa chakavu kabisa lakini sasa wanafunzi wanasomea kwenye madarasa mazuri nay a kuvutia .
Ujenzi wa zahanati ya Kisabi iliyopo Mtongani Mlandizi ulitembelewa pia na kamati ,jumla ya milioni 83 zimetumika katika mradi huu na upo katika hatua za ukamilishaji.
Kamati pia ilitembelea ujenzi wa madarasa manne shule ya sekondari Mpelumbe Bokomnemela madarasa haya yamekamilika kwa gharama ya milioni 80 fedha za kapu la mama na tayari yamepokea wanafunzi wa kidato cha kwanza 2023.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi alimpongeza mwalimu mkuu wa shule hii kwa usimamazi mzuri wa fedha za serikali na kuagiza walimu wakuu wengine wenye miradi wakajifunze kutoka Boko
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.