Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za jamii Halmashauri ya Wilaya Kibaha Mhe. Shomari Mwinshee ameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa inayoifanya ya kusogeza huduma karibu na wananchi.
Shomari ametoa pongezi hizo Jula 27wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo kwa robo ya nne ambapo walitembelea katika Hospitali ya Wilaya na kukagua vifaa tiba vilivyonunuliwa katika hospital hiyo.
Hospitali hiyo ya Wilaya ilipokea miln. 100 kwa ajili ya kununua mashine ya macho na meno .
Amesema kabla ya kujengwa kwa Hospitali hiyo huduma za macho na meno zilikuwa zinatolewa kwenye kituo cha afya Mlandizi jambo lililosababisha msongamano mkubwa kwenye kituo hicho.
" Sasa wananchi watapata huduma hizo kwenye Hospitali ya Wilaya tunaipongeza sana Serikali ya awamu ya sita " amesema Shomari.
Shomari pia amempongeza Mganga Mkuu wa Wilaya pamoja na wataalamu wa afya kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwahudumia wananchi pamoja na changamoto mbalimbali walizonazo na kuahidi kufanyia kazi na zilizo nje ya uwezo watazifikisha ngazi za juu.
Pamoja na hayo Shomari amewapongeza wakuu wa idara za afya, elimu na maendeleo ya jamii kwa kufanya kazi kwa juhudi kwani ndani ya mwaka mmoja akiwa mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii amefanya kazi kwa ushirikiano na wataalam hao na kuweza kupata mafanikio makubwa ikiwemo kufungua Zahanati ya Msufini na Mpiji stesheni.
Naye Mjumbe wa kamati hiyo Mhe. Paul amempongeza Afisa Elimu Msingi pamoja na timu yake kwa kazi nzuri waliyofanya katika kusimamia ujenzi wa madarasa ya BOOST mradi ambao wameukagua na kujiridhishwa na ubora wa ujenzi wa vyumba vya madarasa ambavyo vineonyesha thamani ya fedha.
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.