KIBAHA DC YAPONGEZWA KWA USIMAMIZI MZURI WA FEDHA ZA MIRADI
Kamati ya Siasa Mkoa wa Pwani wamefanya ziara ya kukagua mradi wa Hospitali ya Wilaya ya Kibaha, Akiongea wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Pwani Mhe. Ramadhani Maneno ameipongeza Halmshauri ya Wilaya ya Kibaha kwa kusimamia vizuri fedha za miradi zinazoletwa kwenye Halmashauri hiyo.
“niwapongeze kwa ujenzi wa Hospitali kwa kweli value for money imeonekana hongereni sana, endeleeni kuchapa kazi tunawategemea sana bila ninyi sisi hatuwezi kwenda “alisema Maneno.
Aidha Maneno alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge kufanya mawasiliano na LATRA ili ipatikane route ya magari inayopita kwenye hospitali ya wilaya ili kuondoa changamoto ya usafiri kwa watumishi na wananchi wanaoenda kupata huduma kwenye hospitali hiyo.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge aliieleza kamati hiyo kuwa wamepokea kiasi cha bilioni moja zilizotokana na tozo za miamala ya simu kwa ajili ya ujenzi wa vituo vine vya afya .
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.