Kuelekea miaka 61 ya Uhuru watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha wamezindua kampeni ya upandaji wa miti Leo tarehe 7/12/2022 katika jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha lililopo Kisabi Mlandizi ambapo kila kila mtumishi amekabidhiwa mti wake atakao utunza .
Afisa misitu wa Halmashauri Christina Samweli Ameeleza umuhimu wa upandaji wa miti pamoja na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi hivyo alisisitiza watumishi wote kuwa miti waliyokabidhiwa wahakikishe kuwa wanaitunza na inakua ili kuweza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Khadija Haule kwa niaba ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya kibaha amesema wataihudumia kuitunza na kuijali miti hiyo kwani miti inafaida kubwa kama kupendezesha jengo kuleta kivuli pia kuondoa msongo wa mawazo.
Jumla ya miti 52 imependwa kuzunguka jengo la Halmashauri na miti 300 imepandwa katika ofisi za kijiji za saidi Domo pamoja na ofisi ya chama cha mapinduzi za kitongoji hicho na barabara zake.
"Mti wangu mazingira yangu Taifa langu kazi iendelee"
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.