Jumla ya miradi 99 ya maendeleo ambayo imetembelewa na mingine kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi katika Mkoa wa Pwani imefanikiwa kupitishwa yote bila ya dosari yoyote na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2023.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge wakati akimkabidhi rasmi Mwenge wa Uhuru 2023 kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Robert Chalamila katika eneo la tazara na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa chama pamoja na serikali.
Kunenge alibainisha kwamba mbio za Mwenge wa uhuru ukiwa katika mkoa wa Pwani umeweza kukimbizwa umbali wa kilometa zipatazo 1201 katika Wilaya saba na halmashauri tisa.
Alifafanua kuwa katika miradi hiyo mbali mbali ya maendeleo imegusa sekta mbali na imegharimu jumla ya kiasi cha shilingi trilioni 4.4 ambazo zimetoka serikali kuu, Halmashauri na nyingine kwa wadau wa maendeleo.
Kunenge alibainisha kuwa katika mbio hizo miradi tisa ilifunguliwa,miradi 15 ilizinduliwa , miradi 20 iliwekewa mawe ya msingi na miradi 15 ilikaguliwa.
"Tunashukuru tumemaliza salama kukimbiza mbio za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wetu wa Pwani na miradi yetu yote imeweza kupitishwa bila ya kuwa na dosari yoyote Ile kutokana na kuwa na vigezo ambavyo vinatakiwa,"alisema Kunenge.
Kwa Upande kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Abdalah Kaim alitoa pongezi kw a Mkoa wa Pwani kwa usimamizi mzuri wa miradi na kuwata waendelee kumsaidia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kusimamia miradi ya maendeleo ili iweze kuleta tija kwa wananchi wote
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.