MKUU wa Wilaya ya Kibaha Sara Msafiri ameandaa mashindano ya kuwania kombe la sensa ambayo yanalenga kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhesabiwa .
Akizungumza jana mjini Mlandizi katika kikao chake na baadhi ya Viongozi wa soko, bodaboda na wa daladala Msafiri alisema timu kutoka katika kata 28 za wilaya hiyo zitashiriki mashindano hayo.
Alisema timu sita, tatu kutoka Halmashauri ya Kibaha Mjini na nyingine Halmashauri ya Kibaha Vijijini zitakutanishwa kupata mshindi wa kwanza, wapili na watatu.
Mkuu huyo wa Wilaya alisema timu itakayoibuka mshindi katika mashindano hayo itapeleka kombe la sensa Ikulu kumkabidhi Rais Samia Suluhu Hassan.
Ili kufanikisha mashindano hayo Mkuu huyo wa Wilaya aliahidi kusambaza mipira kwa timu zitakazoshiriki.mkuu
Baadhi ya washiriki wa kikao hicho walimuomba Mkuu wa Wilaya kuandaliwa vipeperushi na fulani kwa ajili ya kuhamasisha na kutoa elimu kuhusiana na umuhimu wa sensa.
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.