Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe. Nickson John amewataka wahudumu wa afya kutoa elimu ya uelewa wa chanjo kwa wazazi wanapowapeleka watoto kupata chanjo ya kwanza ili wazazi waone umuhimu wa kuwapeleka watoto kupata Chanjo zote zinazotakiwa.Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo kwenye kikao cha Chanjo ngazi ya Wilaya kilichofanyika Leo tarehe 25.04.2023 katika ukumbi wa Halmashauri. Akiongea kwenye kikao hicho mratibu wa chanjo Wilaya Khadija Telacky amesema mwitikio wa chanjo ya kizazi ni mdogo sana kwani mabinti wengi wakishapata chanjo moja Hawarudi kumalizia chanjo iliyobaki.Khadija amewataka wazazi kuhakikisha watoto wao wanakamilisha ratiba za chanjo.Pia Khadija amewasisitiza wajumbe kufikisha ujumbe kwa jamii kwamba chanjo hazina madhara bali ni kinga kwa jamiii hivyo ni muhimu kuhakikisha watoto wanamaliza ratiba za chanjo ili kuepuka milipuko.Aidha Khadija amesema wiki ya chanjo imeanza tangu tarehe 24.04.2023 na itafika ukomo tarehe 30.04.2023 hivyo amewataka wazazi kuwapeleka watoto wote na Mabinti kuanzia miaka 14 kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kupata chanjo
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.