Meneja wa NMB kanda ya Dar es salaam Donatus Richard amekabidhi komputa mbili kwa Halmashauri ya wilaya ya kibaha ikiwa ni mchango wa watumishi wa kanda hiyo inayohudumia Dar es salaam na Pwani.
Akiongea wakati wa kukabidhi vitendea kazi hivyo Donatus amesemawatumishi wa kanda hiyo wamechanga fedha kwa ajili ya kulipia gharama za matibabu ya watoto katika taasis ya Jakaya Kikwete(JKCI) jumla ya milioni tano, pia wamelipia bima ya afya kwa watoto yatima 100, pamoja na kununua komyuta 20 kwa ajili ya halmashauri 14 za Pwani na Dar es salaam ambapo Halmashauri ya wilaya ya Kibaha Imenufaika na Kompyuta mbili.
Aidha Donatus ameta wito kwa Watanzania kutumia bank ya NMB wanapohitaji huduma za kibenki kwani benki hiyo inafanya zaidi ya kutoa huduma za kifedha wanatoa huduma za kusaidia jamii pia kwani bank hiyo inatenga asilimia 1% kila mwaka kwa ajili ya kurudisha kwa jamii mwaka jana bank hiyo ilitenga kiasi cha bilioni 2.9.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Butamo Ndalahwa amewashukuru wafanyakazi wa NMB kanda ya Dar es salaam kwa uungwana waliounyesha kwani wametoa mapato yao ya mfukoni ili kuisaidia jamii inayowazunguka .
Butamo amezitaka taasis nyingine ziige mfano wa bank ya NMB na amewaahidi kuwa watazitunza vizuri komputa hizo ili ziweze kuleta tija kwa jamii inayohudumiwa na halmashauri hii.
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.