• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kibaha District Council
Kibaha District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
        • SP FINAL DRAFT
      • Mazingira na Usafishaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maji
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Ufugaji wa Nyuki
      • Uchaguzi
      • TEHAMA
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Maji
    • Afya
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya kisheria
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa halmashauri
    • Kamati za kudumu
      • Fedha Uchumi na Mipango
      • Maadili
      • UKIMWI
      • Huduma za Jamii
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Samia Awataka Watanzania Kuthamini Bidhaa za Ndani

Posted on: October 29th, 2018

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Samia Suluhu amewaasa watanzania kujenga utamaduni wa kununua bidhaa zinazozalishwa kwenye viwanda vya ndani pamoja na wawekezaji  kununua malighafi za viwanda vilivyopo nchini .

Aidha ametoa rai kwa wadau na taasisi zote zinazosimamia miundombinu wezeshi ,uzalishaji na huduma ,kuweka mkakati madhubuti ambayo inaweza kuweka mazingira wezeshi kwa ustawi wa viwanda .

Samia aliyasema hayo wakati akifungua maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya mkoa wa Pwani ambayo yatafungwa Novemba 4 mwaka huu .

Pamoja na hayo ,ameuelekeza mkoa wa Pwani kutumia wawekezaji kuboresha chuo cha ufundi cha Kongowe ili wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano waweze kwenda kupata ujuzi na baadae wapate ajira kirahisi viwandani .

Samia alisema ,watanzania na wawekezaji wa ndani wamekuwa hawana kasumba ya kununua vya kwao ambapo wamekuwa wakikimbilia bidhaa zinazotoka nje ya nchi .

Alieleza ,taswira ya uchumi wa viwanda wa viwanda inahusisha mnyororo mzima kuanzia uzalishaji ,utunzaji na usafirishaji wa malighafi kutoka kwenye maeneo ya uzalishaji hadi viwandani ,uchakataji  usindikaji ,ufungishaji wa bidhaa na usafirishaji wake kutoka viwandani hadi kwa walaji .

Samia alisema ,ili mnyororo huo ufanikiwe inahitaji miundombinu wezeshi na saidizi kama vile umeme,maji ,barabara na mawasiliano pia raslimali ,mifumo ya kitaasisi ,sheria na huduma za kifedha .

“Katika kulijua hili serikali kupitia taasisi mbalimbali ikiwemo TRL,Dawasa na Tanesco sasa zinajielekeza nguvu katika mkoa wa Pwani kuhakikisha umeme,maji ,miundombinu inakuwa ya uhakika ,ili mnyororo wa uchumi wa viwanda uwe vizuri zaidi”alisema Samia.

Kuhusu vijana aliwahimiza kusoma ili kupata ujuzi kwa lengo la kuajiriwa kuliko kutegemea kazi za vibarua .

Alizitaka sekta zinazoshughulikia maslahi ya wafanyakazi wazunguke kuona jinsi wafanyakazi wanavyohudumiwa .

” Wafanyajazi wengine wana wanafanyakazi za uzalishaji bila kupumzika huko viwandani ,masaa ya kazi yanajulikana ,hivyo haki na maslahi yao yapatikane “alifafanua Samia .

Nae waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji ,Charles Mwijage alisema Tanzania inajenga uchumi wa Kitaifa ,ifikapo 2020-2025 wastani wa kipato cha mtanzania iwe milioni 7.5 kwa mwaka .

Aliupongeza mkoa wa Pwani kwa kutoa ajira  za moja kwa moja 20,000 kwa kipindi cha miaka mitatu .

“Ukitaka soka nenda Brazil ,ukitaka viwanda nenda Pwani “alisema Mwijage.

Mwijage alisema kuwa, Tanzania inatumia saruji tani milioni 4.8 kwa mwaka alimhakikishia Samia kwasasa wanauwezo wa kutengeneza saruji milioni 10.8 ,wanauwezo mkubwa kuzidi mahitaji .

Awali mkuu wa mkoa huo ,mhandisi Evarist Ndikilo alisema makamu wa Rais alikuwa mkoani hapo kwa siku tano ziara ambayo imeleta tija kwa wanaPwani .

Alisema maonyesho hayo yataweza kufungua soko zaidi kwa viwanda kwa kujitangaza .

Ndikilo alisema mkoa una jumla ya viwanda 429 ambapo vikubwa na vya kati 109, vidogo 320 na vya kusindika vipo 86 .

Alitaja changamoto inayozikabili baadhi ya viwanda kukosa soko la uhakika hali inayosababisha kusuasua kwa uzalishaji .

2018-10-29

Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili June 28, 2022
  • KUITWA KWENYE MAFUNZO YA SENSA KIBAHA DC TAREHE 29-07-2022 July 27, 2022
  • Tangazo la nafasi za kazi May 27, 2022
  • TANGAZO KWA WATUMISHI AJIRA MPYA July 04, 2022
  • Angalia Vyote

Matukio mapya

  • Kamati ya Fedha Mipango na Uongozi Imefanya ziara ya Kukagua miradi

    July 25, 2022
  • Wakulima wa Korosho Wameomba Serikali Iwasidie Kudhibiti Wizi wa Korosho Mashambani

    July 08, 2022
  • Halmashauri ya Wilaya ya kibaha Imefanya Maadhimisho ya siku ya afya ya Kijiji

    July 05, 2022
  • Waliosababisha Hasara Katika Hoja za Ukaguzi wa Mahesabu Wachukuliwe Hatua -Rc Kunenge

    June 16, 2022
  • Angalia Vyote

Video

Hotuba ya Rais Magufuli wakati wa Kuzindua bunge
Video Nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TOVUTI YA MKOA WA PWANI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA AJIRA
  • TOVUTI YA WANANCHI
  • TOVUTI YA BARAZA LA MITIHANI
  • TOVUTI YA WIZARA YA AFYA
  • TOVUTI YA EWURA

Tovuti Zinazoshabihiana

  • TAMISEMI
  • MKOA WA PWANI
  • TANZANIA
  • AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

Free Visitor&Stat Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    KIBAHA DISTRICT COUNCIL

    Anwani ya Posta: P.O BOX 30153

    Simu ya Mezani: +255 23240224

    Simu: +255 0767520048

    Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM)
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.