Walemavu mfano group cha Kata ya Kawawa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha wamemshukuru Mhe.Samia Suluhu Hassan na serikali ya awamu ya sita kwa ujumla kwa kuwazesha kupata mkopo wa milioni 17 kutoka Halmashauri ya Wilaya Kibaha.Wanakikundi hao wametoa pongezi hizo kwenye maonyesho ya nane nane Kanda ya Mashariki walipotembelewa na Katibu Tawala Wilaya ya Kibaha Moses Mwagoga.Zahara Said Mteri amemwambia Katibu Tawala kuwa walipokea mkopo wa milioni 17 kutoka Halmashauri na wameutumia kuendesha biashara yao ya kilimo cha uyoga.Zahara amesema kilimo hicho cha uyoga kinawasaidia kuendesha maisha yao na kimewasaidia kuondokana na maisha ya kutegemea msaada."Ulemavu sio kushindwa tuna hisia Sawa na wengine " amesema ZuhuraKatibu Tawala amewapongeza wanakikundi hao kwa kuamua kufanya kazi na hii imedhihirisha kuwa walemavu wanaweza kufanya kazi na kuacha kuwa wategemezi.
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.