Wanakikundi cha wisdom wamemshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Tanzania kwa kuwazesha kupata mkopo wa asilimia kumi uliowawezesha kuchimba mabwawa ya samaki na kuanza ufugaji wa samaki.Wajasiriamalia hao wadogo wadogo wameyasema hayo kwenye maonyesho ya nane nane Kanda ya mashariki yanayofanyika Mkoani Morogoro."Tunamshukuru sana Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Tanzania kwa kutupatia mkopo wa milion 7 kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha. Mkopo huo umetusaidia kutuinua kiuchumi kwani tunafuga samaki aina ya Sato. Tunawakaribisha watu wote waje kwenye banda la Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Kuja kujifunza ufugaji wa samaki " alisema Oliver mwanakikundi cha wisdom kutoka Mlandizi.
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.