Mkurugenzi mtendaji wa H/W ya Kibaha Bi. Tatu Selemani, amefurahishwa na kitendo cha wananchi wa Mlandizi kushirikishwa katika ujenzi wa jengo la kisasa la ofisi za H/W ya Kibaha unaoendelea hivi sasa katika eneo la Kisabi.
"Kwa hakika wananchi wamenifurahisha sana kwa kuchangamkia fursa hii" alisema.
Hii ni baada ya kutembelea katika eneo la ujenzi na kushuhudia wananchi wakishiriki vyema katika ujenzi huo, Hata hivyo alisisitiza wananchi wote wanaoshirikishwa kuwa waaminifu na walinzi wa vifaa vya ujenzi ili kuwawezesha wakandarasi (SUMA JKT) kufanya kazi yao kwa ufanisi.
Aidha ujenzi huu utagharimu zaidi billioni 2.7 hadi kukamilika kwake , hata hivyo serikali tayari imetoa kiasi cha millioni 900 na itaendelea kuleta kiasi kilichobakia hadi jengo hilo litakapokamilika.
Wananchi watarajie huduma bora zaidi baada ya jengo la ofisi kukamilika kwani sasa huduma zitasogea karibu zaidi ukilinganisha na sasa ambapo wanasafiri hadi mjini Kibaha kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali.
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.