Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa ametembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha lililopo Nane nane Kanda ya mashariki Morogoro. Mhe.Mchengerwa amewapongeza wajasiriamali wote waliopo kwenye banda la Kibaha na ameishauri Halmashauri iwasilishe taarifa za wafugaji nyuki katika ofisi yake ili waweze kupewa mafunzo kwani fedha imetengwa na inasubiri watumiaji.Aidha Mhe.Mchengerwa alifurahishwa na ubunifu wa mapambo ya asili ambapo alielekeza vitu hivyo vipelekwe kwenye shughuli za utalii kwani vinapendwa na vinahitajika sana.
Awali alimtembelea mjasiriamali wa kutengeneza bidhaa za ngozi na kufurahishwa na ubora wa bidhaa hizo.
ReplyForward |
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.